1 Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba yupo nyumbani. 2Watu wengi wakakusanyika, kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. 3Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4Kwa kuwa hawakuweza kumfikisha kwa Yesu kwa sababu ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa juu ya mahali Yesu alikuwa, wakamshusha mtu aliyepooza akiwa amelalia mkeka wake.